MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 2 October 2015

MAKUBWA HAYA HAPA UNESCO NA REDIO ZA JAMII TANZANIA

Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Kijamii nchini (COMNETA), Sekiku Joseph akizungumza katika Kongamano hilo ambalo amesisitiza umuhimu wa viongozi wa Radio za kijamii kuthamini michango ya wafadhili ili iweze kuwa endelevu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limeendelea kuimarisha Redio za Jamii nchini kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara watendaji wa ngazi mbalimbali kwa lengo la kuzifanya Redio hizo kuwahudumia vema wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph amesema kumekuwa na mafanikio tangu mradi huo kuanza miaka mitatu iliyopita chini ya ufadhili wa UNESCO, Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na Serikali ya Uswizi ambapo licha ya kuwajengea uwezo vifaa vya kieletroniki vilitolewa kwa Redio hizo.
Kongamano hilo la mwaka la siku tatu(3) linafanyika katika Kituo cha Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara (ORS), Terat wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara na limewaleta pamoja watendaji wa Redio za Jamii 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar .
“Tunalenga kuwajengea uwezo ili hizi Redio za Jamii zifanye kazi kwa weredi  ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi waweze kushiriki mijadala inayohusu sekta za afya, elimu na kilimo,”amesema Yusuph.
Mshauri na Mkufunzi wa masuala ya vyombo vya habari jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akisistiza jambo katika mafunzo hayo.
UNESCO inafanya kazi kwa karibu na Muungano wa Radio za Kijamii Tanzania(COMNETA)unaongozwa na Mwenyekiti wake Sekiku Joseph.
 Na Mwanaharakati.

No comments: