Hii ni kamati ya ulinzi na usalama ikitembelea majeruhi
wa ajali wakiwa wodi namba 7 katika hospital ya mkoa wa Kigoma wakiendelea
kupatiwa matibabu.
|
Taarifa kutoka mkoani humo inasema kuwa VIJANA sita
waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha
821 JKT Bulombora, wamefariki dunia na
wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jana jioni.
Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Mawezi
Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
"Ni kweli leo majira ya saa moja jioni
tumepokea miili minne ya vijana wa JKT ambao waliketwa hapa tayari wamefariki
na majeruhi 21. "Wengine wa wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea
kuwapa huduma"alisema Dkt Fadhili. Hali za majeruhi mpaka sasa siyo
nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.
"Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia
matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho,
sababu majeruhi wengi hawana fahamu".
Naye kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Ferdinand Mtui
alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na
kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka.
Huku akisema kuwa ajali
hiyo imetokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori hilo la
jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba makreti ya soda na
unga.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment