Kaimu mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Bi
Wendy Massoy, amewataka
wakaguzi wa
ndani watumie weledi kufanya ukaguzi wa kina katika ofisi za serikali
na mashirika nchini, wakati akifungua mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa
ajili ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Wizara ya Fedha.
Bi Massoy
amesema, viwango vya ukaguzi Kimataifa vinahitaji mkaguzi kuhifadhi taarifa
zake za ukaguzi vizuri, ili kuwezesha mkaguzi mwingine kufikia hitimisho moja
kulingana na kazi iliyofanywa na Mkaguzi wa awali.
Programu ya TEAMMATE uwawezesha wakaguzi kuhifadhi
taarifa zake za ukaguzi vizuri hivyo kuwafanya kutii viwango vya ukaguzi Kimataifa, ambavyo
mafunzpo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi hao katika kazi hiyo.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Gerald Mwanilwa amesema kwa kiasi kikubwa
mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imechagizwa na uamuzi wa dhati wa Rais
Jakaya Kikwete, kuimarisha taasisi za utawala bora, maadili na udhibiti,
ikiwemo NAOT.
Bw. Mwanilwa
ameongeza kuwa Rais alifanya hivyo kwa kuboresha sheria, kuongeza uhuru wa
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuongeza uwazi wa taarifa za Ofisi hiyo kwa kupeleka
Ripoti za CAG kwa mara ya kwanza Bungeni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.
Katika
Uongozi wa awamu ya nne, imeanzishwa sheria ya Ukaguzi wa Umma, ambapo serikali
ilitunga Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008 pamoja na kanuni zake za mwaka
2009.
Wakaguzi 65
kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na 24 kutoka wizara ya Fedha wanahudhuria
mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment