MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 20 November 2015

MAGUFULI ATAJA MAZITO BUNGENI, UKAWA WAONDOKA

Akihutubia bunge la 11 katika serikali ya awamu ya tano, rais wa tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli, ametaja mambo makuu na mazito hasa yale aliyokutana nayo katika kipindi kifupi, ambayo anataka yafanyiwe kazi katika kuyapatia majibu ya haraka.
 Ametaja ;- Rushwa; kuwa lazima iondolewe kwa namna yoyote ndipo atakubali na kukubalika,
                  Bandari; kwa kusema kuwa wizi na ubadhilifu uliokuwapo lazima uondoke,
                  Miundombinu; amegusia kuwa ni lazima wananchi wapate maji,barabara na umeme wa uhakika,
                  TRA; Hapo akasisitiza kupatikana kwa kodi halali na kuondoa wakwepaji,
                  Tanesco; amesema atakomesha tabia ya kukatika hovyo na mgawo usio wa lazima,
                  Ujangili; Hili linahusu kuzuia uvushaji malisili kwa wizi na kuweka mipaka na makaazi ya watu,
                  Uduma za afya; vituo vya tiba, dawa, na vifaa vya tiba.
                  Uhamiaji; Kudhibiti ajira kwa wageni na utoaji hovyo wa vibali vya ukaazi,
                  Polisi; Kuondoa kubambika kesi, madai ya askari na makaazi,
                  Kilimo;  Hapa lazima yaende sambamba na uvuvi, viwanda na mazao,
                  Reli; inakwenda sambamba na uboreshaji wa bandari kavu,hakuna kusafirisha mizigo bure,
                  Makundi maalumu; Kuwezesha wazee, watoto, wasanii, wafanyakazi na walemavu. 
Na Mwanaharakati.

No comments: