Mwili wa aliyekuwa mwalimu wa St. Lucky Vicent,Innocent
Papian miaka 25 ambaye ni miongoni mwa watu 35 waliopata ajali may 6 huko
Arusha na kupoteza maisha jana mwili wake umefikishwa wilayani kwao Kyerwa
mkoani Kagera na kuzikwa.
Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey
Mheruka akiwakilisha serikali ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Kagera
na nje ya mkoa katika mazishi ya mwalimu huyo,huku akisema kuwa mwalimu
Innocent enzi za uhai wake alikuwa anaiwakilisha vyema wilaya ya Kyerwa pamoja
na Taifa kupitia taaluma yake ya uwalimu kwani alikuwa mtumishi ambaye hatiliwi
shaka lolote kwenye vyeti vyake.
SAUTI YA MKUU WA WILAYA KARAGWE
Kwa upande wake afisa elimu taaluma mkoa wa Kagera mwl,Fides Munyogwa amesema kuwa mkoa
umepata pengo kubwa maana ni kijana ambaye ndo alikuwa ameingia kwenye taaluma
lakini malengo yake yameishia njiani.
Pia Mwl,Munyogwa amewasihi wananchi kutoingiza imani yoyote
juu ya kifo hicho kwani ni mapenzi ya Mungu badala yake wamuombee apumzike kwa
amani.
"Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe".
MWISHO.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment