MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday 30 June 2017

AUDIO; MARUFUKU KUZUIA WANANCHI KUJIANDIKISHA NIDA KWASABABU ZA VITAMBULISHO



Afisa msajili wa vitambulisho vya taifa NIDA, ambaye sasa yupo mkoani Kagera kusimamia uandikishaji katika manispaa ya Bukoba Bi. Sophia Mfinanga,  amesema kuwa hakuna ulazima wa vitambulisho hivyo, kwasababu kinachoendelea sasa ni utambuzi na uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la makazi.

Ameagiza watendaji wa kata, mitaa kutokuwazuia wananchi wanaojitokeza kuandikishwa, na mwananchi hatakiwi kuondoka na fomu hiyo, badala yake ijaziwe hapohapo kwenye ofisi za kata au mtaa chini ya uangalizi wa mtendaji au mwenyekiti.

Amesema kuwa mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA, tarehe 30/05/2017 ilitoa elimu yaani mafunzo elekezi kwa wenyeviti wa mitaa na ilitoa mafunzo kwa watendaji mitaa na kata ikiwa ni tarehe 9/06/2017,  hivyo uandikishaji utaendelea hadi 15/07/2017, na hakuna kuwazuia kuandika kwa kukosa cheti cha kuzaliwa, viapo pamoja na vitambulisho vingine kama leseni, kadi ya mpiga kura au vyeti vya shule, kwani kama kutakuwa na lazima hiyo wataelekezwa na maofisa wa uhamiaji.
Siku chache zilizopita, Mtendaji wa kata ya Bakoba katika manispaa ya Bukoba na wengine watatu, wameshikiliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Kagera, kwa kuwatoza wananchi shilingi elfu tano katika uandikishaji wa vitambulisho vya taifa.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, mkuu wa Takukuru mkoani Kagera Joseph Mwaiswelo, alisema kuwa  pamoja na kukamatwa kwa mtendaji huyo, pia inawashikiria watu watatu na wanaendelea kuhojiwa.

Alimtaja mtendaji huyo kuwa Marco Mgoe, huku akisisitiza kuwa majina ya wengine yanahifadhiwa kwa sababu za uchunguzi, na kuwa wanatuhumiwa kwa kutoza wananchi shilingi elfu tano kwa ajili ya kupewa fomu za vitambulisho vya taifa wakati wa uandikishaji unaoendelea. 

Na Mwanaharakati.

No comments: