MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 29 June 2017

VIDEO;KITU CHA TOFAUTI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA MSIMU HUU




July 4 mwaka huu umefanyika uzinduzi rasmi wa maonyesho ya sabasaba mkoani Kagera ambapo mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo alifanya uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kagera. 

Akizindua maonyesho hayo ambayo yatafikia kilele july 9 mwaka huu,amewashauri baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo kushirikiana kwa karibu na halmashauli kwa kuwashirikisha kile wanachokifanya ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafanikiwa kwa asilimia kubwa.

Aidha amesema kuwa serikali inatambua changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha biashara yao,ambapo ni pamoja na maeneo ya kufanyia biashara sambamba na mitaji midogo,na kuahidi kuwa serikali inaangalia na kwa jinsi gani itawasaidia juu ya changamoto hizo.

Sanjali na hayo Mh.Kinawilo amesema kuwa muda wowote ndani ya mwezi huu serikali itazindua mpango wa kuendeleza sekita ya kilimo awamu ya pili ambapo mpango huo unalenga kufanya m apinduzi  ili wakulima walime kutoka kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha biashara.

TAZAMA VIDEO YA DC BUKOBA

Na Mwanaharakati.

No comments: