Uzalishaji
wa chai katika kiwanda cha Kagera tea limited, umeshuka kutoka kilo elfu 60 za
chai kwa siku hadi kilo kati ya elfu 30 hadi 45 kwa wiki moja.
Kushuka
huko kumetokana na wakulima kupunguza au kukata tamaa ya kulima zao hilo .
Akitoa
taarifa kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba, mkurugenzi
mtendaji wa kiwanda hicho Dokta Peter Mgimba, amesema kuwa wakulima wametelekeza
mashamba ya zao hilo, kutokana na bei kutopandishwa ikilinganishwa na mazao
mengine.
Baada
ya kusikiliza matatizo ya kiwanda hicho, mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw. Deodartus
Kinawiro, ametoa agizo kwa uongozi wa
halmashauri ya wilaya Bukoba, kubuni mbinu mbadala za kufufua zao la chai kwa wananchi wake, kwa
kuwaletea maendeleo na kuokoa kufifia kwa zao hilo.
Kiwanda
cha chai cha kagera tea limited kimetakiwa kulipa deni la zaidi ya shilingi
milioni 30 wanazodaiwa na gereza la Rwamurumba
ifikapo julai mwaka huu kama ilivyoelekezwa na mahakama.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro mara baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa kaimu Mkuu wa
gereza la Rwamurumba ASP Focus Kagoroba
ambaye amesema kuwa anashangazwa na uongozi wa kiwanda hicho kushindwa
kulipa deni hilo wakati Mahakama imekwishaweka taratibu za ulipaji deni hilo.
Bwana
Kinawiro amesema kuwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo ya
utafishaji wa baadhi ya mali za kiwanda ,uongozi wa kiwanda hicho unatakiwa
kulipa deni hilo haraka iwezekanavyo.
Mkurugenzi
wa kiwanda hicho amekili uwepo wa deni hilo ambapo amesema kuwa atahakikisha
analipa fedha hizo kwa wakati kama ilivyoagizwa.
Aidha
ameongeza kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinadaiwa kiasi cha shilingi milioni
tatu malipo ya wakulima kwa kipindi cha
mwezi mei na amesema kuwa mchakato wa ulipaji wa madeni hayo utafanyika hivi
karibuni ili kunufaisha wakulima wa zao hilo.
Mkuu
huyo wa wilaya ametumia nafasi hiyo kuwataka
viongozi wa chama cha wakulima wa chai mkoani Kagera, kuacha kuwa wanaharakati ,bali
wafanye kazi yao kwa malengo ya kujiletea maendeleo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment