Mtendaji
wa kata ya Bakoba katika manispaa ya Bukoba na wengine watatu, wanashikiliwa na
taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Kagera, kwa kuwatoza
wananchi shilingi elfu tano katika uandikishaji wa vitambulisho vya taifa.
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu, mkuu wa Takukuru mkoani Kagera Joseph Mwaiswelo,
amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa
mtendaji huyo, pia inawashikiria watu watatu na wanaendelea kuhojiwa.
Amemtaja
mtendaji huyo kuwa Marco Mgoe, huku akisisitiza kuwa majina ya wengine yanahifadhiwa
kwa sababu za uchunguzi, na kuwa wanatuhumiwa kwa kutoza wananchi shilingi elfu
tano kwa ajili ya kupewa fomu za vitambulisho vya taifa wakati wa uandikishaji
unaoendelea.
Amesema
kuwa katika uandikishaji huo, fomu zinatolewa bure na serikali, hivyo wananchi
wasidanganyike kutozwa pesa bila ufafanuzi wa kazi yake.
Mwaiswelo
amesema kuwa wanaendelea na kuwahoji watuhumiwa, na ikiwa upelelezi utakamilika
watu hao watafikishwa mahakamani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment