Mbunge wa jimbo la muleba Kusini lililopo mkoani Kagera
Prof.Anna Tibaijuka ameungana na waisilamu na wananchi wa madhehebu mengine
wilayani Muleba katika kusheherekea sikukuu ya EID akiwa mgeni rasmi katika
baraza la EID wilayani humo.
Kufuatia hafla hiyo iliyoandaliwa na Haji Shakiru Kyetema,imeibuka changamoto ambayo kupitia baraza la EID
wilayani humo wamesema kuwa kwa kipindi
walichofunga wamegundua uwepo wa asilimia kubwa ya watoto yatima katika wilaya
ya Muleba na hawapati msaada wowote kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao,huku
wakimuomba mbunge wao kutoa msaada juu ya changamoto hiyo.
Kwa upande wake Prof.Anna Tibaijuka amepokea changamoto hiyo na kumuagiza katibu wake kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya kufanya sense ya kubaini watoto hao ili iwekwe mikakati bora ya kuhakikisha wanasaidiwa
Picha za matukio mbalimbali katika hafla hiyo
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment