MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 27 June 2017

INASIKITISHA; VIFO VYA MAJI WAKATI WAKIONGELEA {BEACH} BUKOBA

 BUKOBA

Siku ya jana waisilamu walikuwa wanasheherekea sikukuu ya EID-EL-FITRI ambapo kwa mkoa Kagera manispaa ya Bukoba ilimalizika kwa majonzi baada ya watoto wawili mapacha kupoteza maisha pindi walipoenda kusheherekea na kuamua kuogelea katika beach ya Gymkana manispaa ya Bukoba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollomi amethibitisha kutokea kwa vifo hivo,na akiwataja waliopoteza maisha kuwa ni Hussein Hamis na Hassan Hamis wakiwa na umri wa miaka 12 na walikuwa darasa la saba,watoto wa askari kitengo cha usalama barabarani mkoani humo.

Aidha amesema kuwa walikufamaji majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini na tano jioni,na walizidiwa maji wakati wakiogelea kitendo kilichopelekea wakitolewa wamekufa.

Sanjali na hayo Kamanda Ollomi amelaani kitendo cha wanaochoma moto nyumba za wakazi wa wilaya Muleba,kijiji Ibila kata mayondwe ambazo mpaka sasa hivi nyumba 13 tayari zimeteketea kwa moto na wananchi bado wanadai hawajui chanzo cha moto huo.

Kufuatia hali hiyo amewataka wananchi kuwa watulivu na kuondoa woga maana tayari jeshi la  polisi wameshapata taarifa na tayari wameanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

TAZAMA VIDEO YA MKUU WA POLISI KAMANDA OLLOMI



Na Mwanaharakati.

No comments: