By Lameck Richard
Mashindano ya kupata washiriki wa Umitashumita Kitaifa yameendelea leo mkoani kagera huku watoto wa shule za msingi mkoani humo wakionyesha viwango vyao kwa lengo la kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo.
Kwa upande wake afisa michezo mkoa wa kagera Kefa Elias
amesema kuwa mpaka sasa maandalizi ni mazuri na wanategemea kuanzia kesho
wanaanza kambi rasmi itakayojumuisha washiriki 109 kutoka wilaya zote za mkoa
Kagera mara baada ya mchujo kufanyika.
Aidha amesema kuwa timu hiyo itaendelea na kambi katika
maeneo yaleyale ya chuo cha walimu Katoke kilichopo wilayani Muleba,ambapo
watakaa hapo kwa siku saba na baada ya kambi watasafiri kuelekea jijini Mwanza
katika chuo cha Walimu Butimba yatakapofanyikia mashindano ya kitaifa,huku
akifafanua kuwa kikosi kitakachoenda kitakuwa na jumla ya wanafunzi 82,wanafunzi wenye mahitaji maalumu 15 na
walimu 12,wote wa mkoa Kagera.
Akiongea kwa niaba ya Serikali afisa elimu taaluma mkoa wa
Kagera Fides Mnyogwa amesema kuwa kufatia hali inayoonyeshwa na wanafunzi wa
sekondari wanaoshiriki mashindano ya UMISETA jijini Mwanza,wanaamin hata hawa
wa shule za msingi watafanya vizuri zaidi kuhakikisha mkoa wa Kagera unarudi na
ushindi.
Mwl,Mnyogwa amewasihi wazazi na walezi kuendelea kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa kuwaruhusu watoto wao kushiriki michezo kwani ni
sehemu mojawapo ya ajira,huku akiongeza kuwa serikali inajitoa kuendesha
mashindano hayo ili kuhakikisha wanaendeleza vipaji vya watoto mashuleni.
Picha za matukio mbalimbali katika mashindano hayo ngazi ya
mkoa…………………………………………………
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment