MULEBA
By Lameck Richard
Ikiwa vikao vya Bunge la bajeti vinaendelea mjini
Dodoma,wabunge mbalimbali wamekuwa wakitoa hoja zao kwa wizara mbalimbali
zinazojadiliwa ambapo na mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Prof.Anna Tibaijuka amekuwa miongoni mwa watu wanaochangia.
Hivi karibuni ametumia dakika kumi kuchangia katika bajeti
ya wizara ya Nishati na Madini ambapo katika hoja zake aligusia neno la “kadri
unavyopanua ndivyo watu wanavyozidi kutamani”,kipande hicho kilianza
kusambaa katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakitumia neno hilo kwa
malengo tofauti na anachodai alikuwa anaimanisha.
Wakiongea na vyombo vya habari kwa nyakati tofauti,baadhi ya
wananchi wa jimbo lake la Muleba Kusini wamempongeza mbunge wao kwa uwakilishi
anaouonyesha kipindi hiki katika kutetea masilahi ya wananchi wake hususani
upande wa wafugaji na wakulima ikiwa ni pamoja na umeme chini ya mradi wa
kusambaza umeme vijini “REA”ambao unatarajia kuanza kwa awamu ya tatu.
Aidha wamesema kuwa
bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa barabara katika
baadhi ya maeneo na uhaba wa vituo vya afya hususani kata ya Biirabo ambapo
wamemuomba kuweka nguvu zaidi katika sehemu hizo ili waweze kuepukana na
changamoto hizo.
Sanjali na hayo,wameongeza kuwa kuna faida kubwa mbunge
kutokuwa waziri maana awamu hii wameona jitihada alizonazo na anavyojitoa
kuongea bungeni kwa kutetea jimbo lake tofauti na awamu iliyopita wakati akiwa
mbunge na waziri na kumuomba asikatishwe tamaa na baadhi ya watu ambao wanabeza
kile anachokifanya badala yake aangalie wananchi wamekwama wapi ili aonyeshe
msaada wake.
TAZAMA WALICHOKIONGEA
WANANCHI HAO KATIKA HII VIDEO……………………………………………..
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment