MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 3 June 2017

ALICHOSEMA MWENYEKITI WA HALMASHAURI BUKOBA

Diwani wa Rukoma na Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze, ameaahidi kutoa vifaa vya michezo kwa Timu ya Tarafa Rubale, ikiwa ni pamoja na Mipira na Jezi.

Ahadi hiyo imekuja mara ya baada ya kufikishiwa kilio cha Timu hiyo ya Rubale Fc, Na mwakilishi wa timu hiyo Ndg, Abdullatif Yunus (Dulla), katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Katani Rubale.

Akiwasilisha ombi hilo Dulla, amemuomba Mwenyekiti  huyo kuwa Timu ya Rubale Fc, ni Timu yenye kujitahidi katika maendeleo ya Soka ndani  na nje ya Tarafa Rubale, ikiwa ni pamoja nakucheza mechi mbalimbali za kirafiki na kushinda, lakini changamoto kubwa imekuwa ni kuazima jezi kila inapofika wakati wa kucheza mechi hizo, hivyo kumuomba Mh. Ngeze kuisaidia jezi katika kuinua na soka. 


Wakati huo huo wakaazi wa kijiji cha Bituntu kwenye kata hiyo, wameomba mwenyekiti huyo kuwezesha ujenzi wa barabara ili waweze kuzifikia huduma kwenye kata ya karibu ya Izimbya.
Na Mwanaharakati.

No comments: