MULEBA
By Lameck Richard
Kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kata ya
Kalambi jimbo la Muleba kusini chini ya Diwani wa kata hiyo,Felix Bwahama
umekuwa na matukio mbalimbali likiwemo la
viongozi wa vijiji na kitongoji
kutoka Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuhamia chama cha
mapinduzi CCM.
Viongozi waliohama ni pamoja na mwenyekiti kijiji kalambi
Anton Bajuza,mwenyekiti kijiji Kanyamita Mseveni Kazinja na mwenyekiti wa
kitongoji Bushabo Sebastian Rutakakwa,ambapo wamesema kuwa sababu kubwa za
kuhamia CCM ni kutokana na uongozi mzuri walionao wa diwani wao pamoja na
ushirikiano mkubwa wa maendeleo wanaoupata kutoka kwa diwani,mbunge pamoja na
Rais.
Kufuatia kitendo hicho Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya
ya Muleba Anatory Nshange amewapongeza kwa hatua hiyo ya kuamua kuungana na
chama tawala katika kuwaletea wananchi maendeleo huku akimuagiza katibu wa ccm
kata Kalambi kujadili haraka majina ya
watu hao ili waweze kupatiwa kadi za chama rasmi.
Sanjali na hayo Diwani wa kata hiyo Felix Bwahama,amezitaja
shughuli za maendeleo ambazo wamefanikiwa kutekeleza ndani ya kata yake kwa
kushirikiana na wananchi pamoja na wafadhiri mbalimbali kuwa ni pamoja na
kukarabati miundombinu katika shule za kata hiyo,zahanati,umeme vijijini na
kufanikiwa kupata barabara ya rami km 10 kutoka Kimea-Nyamilanda.
Kwa upande wa wananchi wamebainisha changamoto wanazokumbana
nazo kuwa ni pamoja na ukosefu wa maji katika kata yao hali inyopelekea kufuata
maji kwa umbali mrefu na kusababisha shughuli nyingine za maendeleo kukwama.
Aidha wameongeza kuwa wanaiomba serikali iwape idadi ya
mifugo wanayotakiwa kuwa nayo kama wafugaji na kutengewa maeneo ya kuchungia ili
kuepukana na adha ya kuvutana na serikali
kila wakati.
Bw.Bwahama amesema kuwa watendaji wa kata na vijiji
wahakikishe wanasimamia vyanzo vya maji kwa ukaribu na wasiruhusu mtu mmoja
kuharibu vyanzo hivyo kwa sababu maji ni changamoto kubwa na yanategemewa na
watu wengi,huku akisema kuwa bado anaendelea kupambana katika halmashauri ili
wajengewe visima vya chini na tayari kuna kijiji kimeshawekwa kwenye mradi.
Pia amewasihi viongozi na watendji wa kata hiyo
kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza wajibu wao na kuwaomba wananchi
kutoa ushirikiano pindi wanapokumbana na changamoto hiyo ili hatua ziweze
kuchukuliwa dhidi yao.
TAZAMA HAPA KWENYE VIDEO ALICHOKISEMA DIWANI WA KATA KALAMBI
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment