MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 2 June 2017

SWALI JUU YA ASKARI KUATHIRIKA WAKATI WA UTEKETEZAJI BANGI LAZUA MJADALA BUNGENI

Swali hilo limeulizwa na Mbunge Ester Matiko kuwa kuna athari gani wakati askari wakitekeleza uchomaji wa bangi na je hiyo haiwezi kuwa sababu ya askari kufanya kazi kinyume na taratibu?

Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dr. Khamis Kigwangala, amejibu kuwa mara zote askari wanatakiwa kutumia vifaa vya kujifunika, na kama hawavai, moshi wa bange hauwezi kusalia mwilini mwa binadamu zaidi ya siku 30 labda wakifanya mwendelezo wa uvutaji.

Wakati huo huo waziri wa kazi, ajira na vijana Jenister Mwagama, amefafanua kuwa serikali inaamini kuwa askari wanatumia weledi wakati wa uchomaji wa bangi au mashamba, kwa kuzingatia mwelekeo wa upepo hivyo wanaamini kuwa hakuna athari wanayokutana nayo.

Mara nyingi kumekuwa na matukio ya utekelezaji wa mashamba ya bangi, kuishirikisha askari na raia wakiwa katika wingu kubwa la moshi ambao unatajwa kuwa na madhara kwa binadamu.
Na Mwanaharakati.

No comments: