MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 2 June 2017

MJADALA MPYA JUU UTUNGAJI VITABU WATIKISAA

Shirika la TWAWEZA limeungana na wadau wengine kushauri serikali kusimamia au kuweka utaratibu mpya wa mfumo wa utungaji vitabu vya kujifunzia na kufundishia.

Akizungumza kupitia Azam TV, siku moja baada ya chama cha wachapishaji binafsi na baadhi ya wadau kulalamikia vitabu vyenye makosa ya kisarufi Bi.   Zaina Mgala meneja idara UWEZO  kutoka shirika la TWAWEZA, ameonesha moja ya kitabu miongoni mwa vile vyenye makosa mbalimbali kwa kueleza baadhi ya maneno yenye makosa kisarufi hasa kwenye lugha ya kingereza.

Itakumbukwa kuwa uliwahi kuibuliwa mjadala juu ya mitaala ya elimu mwaka 2013 ambayo ilianzishwa na mbunge wa Vunjo James Mbatia ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa kuteuliwa, alipopeleka hoja bungeni ukitaka serikali kufanya juhudi za makusudi kushughulikia mitaala na utunzi huo wa vitabu.

Kwa pamoja sasa wanasema hali ikiendelea kama ilivyo hakuna mabadiliko ya msingi yatakayopatikana, ulitolewa mfano wa kitabu kimoja cha kingereza darasa la tatu kuwa ukurasa wa tatu kumeandikwa listen and show the colours of national Frug.

Na Mwanaharakati.

No comments: