Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza rasmi kuondoa nchi yake katika mkataba wa makubaliano ya mataifa tajiri duniani, kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutokana na maendeleo yake makubwa kiviwanda.
Akihutubia kupitia vyombo mbalimbali vya habari duniani, Trump amesema kuwa alishaahidi kuismamia Marekan na sasa anatekeleza kwani lazima kuiweka nchi mbele kama rais, kuangalia maslahi ya watu wake.
Jumamosi iliyopita, mataifa yaliyoondelea zaidi kiviwanda G7 yalikutana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kuthibitisha makubaliano yao ya miaka miwili iliyopita mjini Paris Ufaransa, ambapo kansela wa Ujeruman Angela Makel na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, walishauri Trump kutoiondoa nchi yake bila makubaliano, baada ya Trump kuahidi kutoa jibu baada ya wiki moja tangu mkutano huo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment