BUKOBA
Ikiwa leo ni kilele cha wiki ya maziwa kitaifa ambapo
imefanyika mkoani Kagera katika viwanja vya Kyakairabwa manispaa ya Bukoba,huku
waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Dr.Charles
Tizeba akihitimisha maadhimisho hayo kwa niaba ya makam wa Rais Samia Suluhu.
Akisoma hotuba kwa niaba ya makamu wa Rais,Dr.Tizeba amesema kuwa pamoja na
Tanzania kuwa na idadi kubwa ya uzalishaji maziwa bado unywaji wa maziwa
umeendelea kuwa mdogo ambapo mtanzania mmoja unywa lita 47 kwa mwaka badala ya
lita 200,jambo ambalo linapelekea kuwepo ongezeko kubwa la magonjwa ikiwa ni pamoja
na lishe duni.
Dr.Tizeba amesema kuwa nchini Tanzania imedhihirika kuwa vifo
130 kwa watoto wa chini ya miaka mitano hutokea kila siku kutokana na lishe
duni,hii ni kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF
kwa mwaka 2013.
Mbali na kuhitimisha maadhimisho hayo amezindua operation
inayoitwa jenga jahazi,jenga afya,jenga uchumi kupitia maziwa ambayo ina lengo
la kuendelea kuhamasisha watanzania kunywa maziwa ili kupunguza tatizo la udumavu
wa mwili na akili hususan kwa watoto wetu.
Sanjali na hayo
amekabidhi vyeti,medali na vikombe kwa waliofanya vizuri katika maadhimisho ya
awamu hii na mshindi wa jumla ni Kampuni ya ASAS DAIRIES LTD kutoka Iringa
ambao mpaka sasa wamekuwa washindi mara tano mfululizo katika maadhimisho ya
wiki ya maziwa.
Baada ya kuibuka mshindi wa jumla,mkuu wa Kampuni hiyo ya
ASAS DAIRIES Lipita Memila amesema kuwa pamoja na kuendelea kufanya vizuri katika bidhaa
zao,bado wanasaidia jamii kupitia kile wanachokipata ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa wodi katika hospitali mbalimbali na huduma nyingine za kijamii.
BAADHI YA PICHA NDANI YA KILELE CHA WIKI YA MAZIWA KITAIFA
Maandamano ya wanafunzi na wadau mbalimbali katika kilele cha wiki ya maziwa 2017
Add caption |
Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi akinywa maziwa
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment