Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Tayari amewasili Mkoani Kagera katika Kilele cha
Wiki ya Maziwa, Maadhimisho ambayo yamekuwa yakiendelea Takribani wiki nzima
sasa, katika Manispaa ya Bukoba katika viwanja vya Kyakairabwa.

Baada ya
kuwasili uwanja ndege na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh, Deodatus
Kinawiro, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, msafara umeelekea Viwanjani Kyakairabwa
ambapo huko ndipo shughuli inapofanyika.
Waziri
Tizeba, mara baada ya kuwasili viwanjani hapo, amepokea maandamano ya wadau wa
maziwa wakiongozwa na wanafunzi pamoja na walimu wao kutoka shule mbalimbali za
manispaa ya Bukoba, kisha kuanza kukagua na kutembelea mabanda mbalimbali.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment