MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 1 June 2017

MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI KWA NJIA YA KIELECTRONIC, NA KAULI NZITO YA WAZIRI WA FEDHA





Waziri wa fedha na Mipango Philp Mpango, amemweleza rais Magufuli kuwa amechoshwa na serikali kuwa ombaomba.

Dr. Mpango amesema hayo   wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ukusanyaji kodi kwa njia ya kielektroniki  jijini Dar es salaam, ambapo rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi, kuwa haiwezekani serikali ikaendelea kuomba mikopo ya kutekeleza mambo yake ambayo hatahivyo, yangeweza kutekelezwa kupitia fedha zake za ndani.

Amesema kuwa ili kuhakikisha hilo, kama waziri atahakikisha anasimamia mfumo huo unaozinduliwa leo ili uweze kuongeza ukusanyaji wa mapato nchini.

Mfumo huo ulianzishwa mwaka 2015 kwa kumwezesha mlipa kodi kulipa katika benki mbalimbali kupitia simu ya kiganjani, pamoja na wa forodha unaowezesha kulipia mizigo maeneo ya forodha kwa lengo la kurahisisha ulipaji wa kodi ya mizigo kwenye ofisi ya forodha, ili kuondoa ukwepaji wa kodi na kuisbabaishia serikaili hasara, kwani inategemea mawasilisho ya makadirio kutoka kampuni husika, ili kutoipunja serikali au kuwapunja walipa kodi.

Akitoa taarifa ya mfumo huo, kamshina mkuu wa mamlaka ya mapato nchini TRA  Charles Kicheere, amesema kuwa utakuwa unakusanya ongezeko la thamani, kutoka kwenye mialama mbalimbali, kuahikikisha kodi inakaridiwa na kufikishwa kwenye mamlaka husika.

Hotuba ya rais wa jamhuri ya Muungano inaendelea katika uzinduzi huo kwenye ofisi kuu ya mfumo wa ukusanyaji kodi ya TRA Kijitonyama jijini dare s salaa, ambao umeudhuriwa na rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, makamu wa rais Samiah Suluhu Hassan, waziri wa fedha na viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini.
 
Na Mwanaharakati.

No comments: