MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 26 June 2017

WALIOTUMIA GARI LA MATANGAZO KUHAMASISHA WAISLAMU KUFUNGUA WATANGAZIWA KIAMA



Shekh mkuu mkoani Kagera Haruna Kichwabuta, amesema kuwa watachukua hatua kwa baadhi ya waislamu waliotangaza kuwa waliofunga jumamosi wamefanya makosa.

Amesema hayo katika ibaada ya Id el Fitri katika msikiti wa Jamiah mjini Bukoba, kuwa hakuna anayemzuia  muislamu mwenzake kuabudu anachotaka, kwani wote ni watu wa mwenyezi Mungu na wanaruhusiwa kuabudu kwa namna wanavyoamini.

Shekh Kichwabuta amesema kuwa kilichofanyika jumamosi kwa baadhi ya waislamu kuzunguka na gari  kutangaza na kuagiza waislamu kufungua siku ya jumapili, kuwa hawana ruksa ya kufanya kilichofanyika kwasababu kila dini ina msemaji wake na kama waislamu wafike hatua waseme sasa basi.

Amesema kuwa huo ni utaratibu usiokubalika kwa kutumia uhuru vibaya kupitia mgongo wa dini, na serikali inapochukua hatua wanalalamika kuwa wananyanyaswa na serikali yao, na kwamba kuna misikiti mingi, hivyo  kila muumini anaswalia anapoona panamfaha kuliko kuvuruga wenzao.

Siku ya jumamosi, Mufti mkuu wa Tanzania Aboubakar Zuebir alitangaza kuwa mwezi haukuonekana, na kama kiongozi alifanya mawasiliano na wezake wa Zanzibar, Kenya na maeneo mengine, na kumweleza kuwa mwezi haukuonekana na kutangaza Id kufanyika siku ya jumatatu.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: