MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 25 June 2017

WALICHOKISEMA JESHI LA POLISI MKOA WA KAGERA JUU YA NYUMBA ZINAZOTEKETEA GHAFLA

MULEBA


Ikiwa ni siku chache imerepotiwa kuwepo hali ya kushangaza katika wilaya ya Muleba kata Mayondwe mkoani Kagera kufuatia nyumba zilizokuwa zikiteketea ghafla kuanzia may 4 mwaka huu na kufikia nyumba 13 mpaka sasa pasipokujua chanzo cha moto huo,hali hiyo imewalazimu jeshi la polisi kupitia mkuu wa upelelezi mkoa wa Kagera kufika eneo hilo.


Mkuu wa upelelezi mkoa Kagera Max Kahindi amewataka wananchi kuwa wapole kufuatia matukio hayo huku akiwataka kutoingiza chuki binafsi badala yake watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha wanajua chanzo na mtu anayechoma nyumba hizo ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Aidha amewasihi wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa za kweli ili kumbaini anayefanya kitendo hicho huku akisema kuwa atakayebainika ametoa taarifa za uongo kwa kumsingizia mtu ambaye hausiki naye pia atachukuliwa hatua.

Pia ameongeza kuwa kitendo kinachofanyika ni kosa la jinai,hivyo anayechoma nyumba hizo aache mara moja kabla hajachukuliwa hatua,na amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wale ambao wameguswa kwa kuwasaidia huduma mbalimbali ikiwemo sehemu ya kuishi kwa muda wakati serikali ikiendelea na upelelezi juu ya matukio hayo.

MWISHO.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: