Shughuli zote
za bunge la 11 mkutano wa saba zimekamilika rasmi, na bunge hilo limeahirishwa
rasmi kwa serikali kukamia kudhibiti na kupambana na wahalifu, kuimarisha
kitengo cha maafa na kutoa elimu kutokana na matukio mazito yaliyotokea nchini
mwishoni 2016 na mwaka huu 2017.
Pamoja na
waziri mkuu kuahirisha bunge hilo litakalorejea septemba 5 2017, mkutano huo wa saba kupitia mwanasheria mkuu
George Massaju, umepitisha mswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka
2017, uliosomwa na kujadiliwa kwa lengo la kuwa sheria za nchi.
Katika hotuba
yake kuhitimisha bunge hilo inayoendelea hivi sasa, waziri mkuu Kassimu
Majaliwa, amesema kuwa serikali imesikitishwa na matukio yaliyotokea wakati
bunge hilo likiendelea, ikiwemo vifo vya wanafunzi na walimu wao wa shule ya
Lucky Visent mkoani Arusha, pamoja na mauaji hasa ya askari 8 waliokuwa kazini
wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Amesema kuwa
tarehe 14 jun bunge lilipitisha azimio la kuunga mkono juhudi za rais juu ya
rasilimali za taifa ikiwemo madini, kwamba hiyo ni hatua nzuri ya kuhakikisha
watanzania na taifa kwa ujumla wananufaika na maliasili za nchi.
Amesema kuwa
usalama wa raia na mali zao ni shwari na serikali kupitia bunge hiloinaahidi
kupambana na uhalifu, ingawa wapo baadhi wanaotaka kuhatarisha usalama wananchi
wenzao, na serikali inaendelea kuchukua hatua za muda mfupi na mrefu ili
kukomesha hali hiyo.
...........MSIKILIZE WAZIRI MKUU HAPA..............
Bunge
lilitarajiwa kufungwa wiki iliyopita, ingawa kwa makubaliano ya wabunge
waliamua kuongeza siku tano kwa lengo la kuwezesha kujadiliwa miswada ya
sheria.
Na Mwanaharakati.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment