Polisi Mkoani Kagera imewakamata
washukiwa wa kwanza wa matukio ya uchomaji moto nyumba zinazofikia 15 mpaka
sasa wilayani Muleba, huku mmoja akikimbia pamoja ilhali kamanda akieleza juu ya watu wengine wakifariki baada ya nyumba yao kuchomwa.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera Augostin Ollo, ameieleza kasibante redio
kuwa watu hao walikamatwa kufuatia tukio lingine la uchomaji nyumba ya mtu
mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Protaz Karuya, mwenye umri wa miaka 60, na
mkaazi wa kijiji Bugasha kata Mayondwe katika halmashauri ya wilaya Muleba.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Badrul Daniel
wa miaka 32, msubi na mkazi wa kitongoji Ibara, na Angela Karisti mwenye miaka 36,muhaya na mkazi wa kitongoji
Bisole kata Muhutwe.
Amesema kuwa kukamatwa kwa watu hao kumetokana
na taarifa za mtu mwenye mahusiano na
mtuhumiwa aliyebainika kujihusisha na tukio la kuchoma nyumba hiyo na
kukimbilia kusikojulikana.
Wakati huo huo polisi mkoani Kagera
inashughulikia taarifa za wanandoa wawili kuungulia kwenye chumba wakiwa wamelala.
Amewataja marehemu hao kuwa ni Rameck Masinde aliyekuwa na miaka 64, na Katarina Lameck mwenye miaka 33, wote wanyambo na
wakazi wa Karagwe katika tukio lililotokea julai pili mwaka huu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment