Madereva kumi kati ya 21 wa Tanzania walikokuwa wametekwa mashariki mwa
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wamefika Morogoro wakitokea mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa afisa biashara mkoani Kagera Isahya Tendega,
aliyezungumza na mwandishi wa macmedianews, amesema kuwa madereva hao kumi
waliingia mkoani Kagera kupitia kwenye halmashauri ya Ngara, walipoingilia juzi
tarehe 6/7/2017, baada ya kutekwa na kuachiliwa na kundi la Mai Mai.
Amesema kuwa madereva hao raia wa Tanzania, walitekwa wakiwa na malori
yenye mitambo ya kuchimba madini, ambapo watekaji waliharibu malori yao kwa
kupasua tairi na kuwanyang’anya vitu vyote walivyokuwa navyo, na hatimaye
kuwaachilia, hivyo wameingia nchini kwa kutembea na kuomba misaada ya hapa na
pale.
Madereva hao waliokuwa wakiendesha malori ya makampuni ya Alistair na Primefuel yote ya Tanzania, walitwkwa juni 29/2017 na kundi la wapiganaji wa Mai Mai, walipokuwa wakielekea kwenye mgodi wa Namoya kwenye jimbo la Mainiema mashariki mwa Congo, unaomilikiwa na kampuni ya Banro gold ya Canada.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ushirikiano wa kikanda
na afrika mashariki, serikali inaendelea kufanya mawasiliano ya karibu na
mamlaka za Congo, kwa lengo la kujua namna ya upatikanaji wa mali
zilizoharibiwa, ilhali ikieleza kuwa madereva wengine 11 wameshapatikana,
hisipokuwa waliokuwa bado wanatafutwa ndiyo hao waliopatikana mkoani Kagera.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment