Kamati ya baraza la madiwani katika halmashauri ya Bukoba imelazimika kuwatoa nje madiwani watatu wa kata Bwendangabo, Rubale na kata Nyakato, baada ya kupinga suala la watumishi wa halmashauri hiyo kuagizwa kuchangia shilingi elfu 3,000 za mbio za mwenge.
Msemaji
wa kundi la madiwani hao Daniel Damiani ambaye pia ni diwani wa kata Nyakato, amesema
kuwa madiwani hao wametolewa kutokana na msimamo wao wa kutokubali hoja ya
malipo hayo, iliyotolewa kwenye kamati hiyo, ingawa zilishawahi kusambazwa
barua za kuwataka watumishi kuchangia shilingi elfu tatu kila mmoja.
.........BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA.................
.........BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA.................
.
Wakati huo huo
tumishi katika halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera, wametakiwa kufanya kazi kwa
mujibu wa sheria katika kutumia fedha za kutekelezaji miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Hayo yamesemwa na
mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodartus Kinawiro, kwenye baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo.
Bw. Kinawiro amesema
kuwa kuna baadhi ya watumishi katika halmashauri hiyo ambao wanafanya kazi kwa
mazoea, hasa watumishi hao ushindwa kuzisimamia fedha zinazotolewa na serikali
na kuelekezwa katika miradi ya idara zao.
Amesema kuwa
serikali ya awamu ya tano haitamvumilia mtumishi yeyote , ambaye ataonekana
kuwa mzigo kwa serikali, na kulitaka baraza la madiwani kuwachukulia hatua
kali, watumishi ambao wataonekana kusuasua katika utendaji wa kazi zao.
Baraza la madiwani
wa halmashauri ya Bukoba, madiwani wamewasilisha taarifa za maendeleo ya kata
zao na kuzijadili.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment