Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa
kuwaua wahalifu wawili ambao ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji
katika Kanda maalumu ya Polisi Rufiji kufuatia operesheni kali
inayoendelea katika Wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji
mkoani Pwani.
Akielezea tukio hilo,
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano
Julai 5 majira ya saa nne usiku katika msitu wa Ngomboroni kata ya
Ikwiriri, Wilaya ya Ikwiriri Kanda maalumu ya Rufiji ambapo askari wa
operesheni maalum wakiwa katika doria za ufuatiliaji wahalifu sugu
wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea katika Kanda hiyo ya kipolisi.
Sabas alisema Askari
wakiwa na mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji hayo ambaye
alikuwa amekamatwa na baada ya mahojiano alikubali kwenda kuwaonesha Polisi
mahali ambapo ni maficho ya wenzake.
Sabas alieleza kuwa, baada ya
kufika eneo la msitu wa Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa
kufikia watano walikurupuka kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia
ndipo askari Polisi kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa
kumjeruhi mhalifu mmoja kwa risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa
aliyekuwa mkononi mwa polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo
kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo idadi yao kufikia wawili.
Majeruhi hao wawili walifariki
dunia njiani wakati wakipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kuvuja
damu nyingi iliyosababishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata. Miili ya
marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
“Katika tukio hilo tumefanikiwa
kupata silaha mbili aina ya SMG na shot gun moja pamoja na
risasi tisa za SMG zilizokuwa kwenye Magazine.” Alisema Sabas.
Aidha, mkuu huyo wa
Operesheni maalum za Jeshi la Polisi Naibu kamishina Sabas
ameendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha
kupatikana kwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba zawadi nono bado ipo
pale pale na itatolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana
na wahalifu wanaojihusisha na mauaji katika kanda maalumu ya Rufiji.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment