Bwana Pastory Kafundi ni mwananchi
mkaazi wa kijiji cha Ngalalambi katika halmashauri ya wilaya Biharamaulo,
ambaye alitumia nafasi yake kuomba rais awasaidie kuchangia ujenzi wa darasa
katika shule ya msingi Mizani, baada ya wanafunzi kusomea chini ya mti tangu
januari mwaka huu.
Akizungumza na macmedianews, mwananchi
huyo amesema kuwa aliamua kujitoa muhanga kumweleza rais suala hilo, baada ya
kuona kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaofikia elfu tatu katika shule hiyo ya
msingi, na hata wengine kusomea chini ya mti ilhali wazazi na walezi
wakiendelea kujitolea kujenga bila mafanikio kutokana na kukabiliwa na kero za
miundombinu ya maji.
.
Mtandao huu umetembelea darasala hilo
chini ya mti na kukuta mwalimu wake akiendelea kufundisha, kwa lengo la kujua
kero anazokabiliana nazo katika ufundishaji wake huo.
Imebainika kuwa analazimika kutumia nguvu nyingi kuwashawishi watoto hao ambao mara nyingi wanapoteza muda kushangaa magari na wapita njia kutokana na mti huo kuwa karibu na barabara.
Wakati akipita katika kata ya Nyakaula,
rais Magufuli alisimamishwa na kundi la wananchi wakitaka asikilize kero zao,
ndipo mmoja wa wananchi aliyejieleza hapo juu, alipojitolea kumweleza rais
hitaji lao juu ya ujenzi wa madarasa, na kumlazimu rais kutoa ahadi ya shilingi
milioni 10 ambazo alizikabidhi kwa mkuu wa mkoa siku akihitimisha ziara yake
Kagera kuelekea mkoani Kigoma.
Akikabidhi fedha hizo kwa uongozi wa shule na
mbunge wa jimbo la Biharamulo, mkuu wa mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu
Salum Kijuu, aliwataka viongozi na wananchi kuzitumia kwa malengo
yaliyokusudiwa, nayeye kuwiwa kuchangia mifuko 10 saruji baada ya kuridhishwa
na ujenzi unaoendelea shuleni hapo Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment