Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya
Biharamulo mkoani Kagera, wamemlalamikia mbunge wa jimbo la Biharamulo,
kutoonekana jimboni kwa kipindi kirefu mpaka rais alipofanya ziara.
Wakizungumza kwa jazba baada ya kumwona
mbunge huyo kwenye mkutano wa rais Magufuli, wananchi hao wamesema kuwa wanazo
kero nyingi ambazo kama angekuwa amezichukua kupitia nafasi yake ya mbunge
zingeshafanyiwa kazi na serikali, hivyo hakuwa na sababu ya kuja wakati wa
mkutano wa rais wala mkuu wa mkoa.
.
Katika maelezo yake kwa wananchi hao
mbunge Oscar Mkasa, amesema kuwa amekuwa
akibanwa na shughuli za kibunge, ingawa mara nyingi amejitahidi kushughulikia
baadhi ya kero za wananchi wake, akitaja mgogoro wa wafugaji wa Miongora kuwa
aliutatua yeye, pamoja na kuomba shilingi milioni 200 za maji, katika mradi
utakaotekelezwa na serikali.
Wakizungumza na mwandishi wa kituo hiki,
wananchi wa kata ya Nyakaula katika halmashauri ya Biharamulo, wametaja kuwa
wanakabiliwa na kero ya ukosefu wa huduma ya maji, uhaba wa vyumba vya madarasa
mpaka kuwalazimu kutaja kero hiyo kwenye mkutanio wa rais, na baadhi yao
kuchukuliwa maeneo kwa kufanyika uwekezaji wa visima vya maji bila fidia.
Bi. Mastula Hamis yeye ardhi yake
ilitwaliwa na uongozi wa kijiji na kujengwa visima vya maji, lakini wakakiuka
makubaliano ya kuwa analipwa kila mwisho wa mwezi na kuandikiwa barua kuwa
atafidiwa eneo lingine ambalo hatahivyo hakuwahi kupewa, huku akizuiliwa
kuwafikia viongozi wa ngazi ya juu mamlakani.
Akiwa ziarani mkoani Kagera, rais wa
jamhuri ya muunagno wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, aliwahidi wananchi
kuwa atamtuma muhandisi wa maji, ili aweze kushughulikia huduma hiyo, kwani
hilo ni jukumu la serikali, na kuchangia shilingi milioni 10 za ujenzi wa darsa
katika shule msingi Mizani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment