Watoto wawili walioungana kuanzaia kifuani mpaka tumboni wamezaliwa
kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Misheni ya Bigwaa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Huku
hali ya mama na watoto hao ikiendelea vyema na mapacha hao wakiwekwa kwenye chumba maalumu kwa uangalizi, ingawa wamezaliwa wakiwa wametimiza
miezi 9 kama kawaida.
Baba mzazi wa watoto hao Luka Kimole amesema kuwa ni suala la kushangaza
kupata watoto kama hao lakini kwakwe katu halichukulii kama mkosi bali
neema ambayo imetoka kwa Mungu.
Kaimu
Mganga mkuu wa hospitali ya Berega anasema kuwa hali hiyo kujitokezakatika miaka ya sasa ni kutokana na malezi ya ujauzito.
"Mara
nyingi akina mama wanapokuwa wajawazito hushauriwa kutumia baadhi ya
huduma za tiba, kwa mfano Ferav na Folic ambazo zinawasaidia kwakiasi
kikubwa kuzuia watoto kuzaliwa katika hali kama hizi lakini katika hili
hatuwezi kuongea zaidi ni uchunguzi zaidi utafanyika kuona ni kwanini
hali kama hzi hujitokeza kwa wingi hasa miaka ya hivi karibuni.
"
Kwa nje waweza kuona kama watoto wawili ni vigumu kujua jeh kwa ndani
ni miili ya wawili tofauti au kuna kitu kimoja kinawaunganisha,
hivyo kuona kama inaweza kufanyika huduma ya kutengenisha.
Na Gsengo
No comments:
Post a Comment