MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 23 July 2017

AUDIO; RAIS MAGUFULI ASISIMUA WATANZANIA JUU YA KAFULILA



Rais wa jamhuri ya muhungano wa Tanzania, amezindua mradi wa maji wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kabla ya kufanya uzinduzi wa barabara ya Kaliua yenye kilometa 56 mkoani Tabora.


Wakati wa uzinduzi huo wa mradi wa maji wa Nguruka wilayani Uvinza, rais Magufuli amesema kuwa mradi huo unaogharibu shilingi bilioni 2.8, ni muhimu wananchi wautunze kupitia viongozi wao, huku akiwahidi wananchi kuwa kama rais ataanza kufanya mipango ya kufikisha huduma ya umeme.


Pamoja na kufanya uzinduzi huo, amemwagiza waziri wa maji Gerson Lwenge, kuwaondoa watumishi wanaokwamisha miradi ya maji kutelezeka haraka, akisema kuwa yeye kama rais ataondoa walioko ngazi za juu lakini wa ndani ya wizara waziri anao uwezo wa kuwaondoa bila hata kumwomba rais ushauri.

Rais Magufuli amempongeza aliyekuwa mbunge wa Uvinza David Kafulila, juu ya kutetea haki za watanzania wasiendelee kuibiwa juu ya kuibua hoja ya IPTL na kuisimamia, kwamba alisimamia wizi huo wa ajabu, ingawa wapo waliombeza na kumtukana kwamba hata kama walimtukana lakini ukweli wake unaonekana.
..........BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA......... 



Amesema kuwa barabara ya kutoka Maragarasi kwenda Uvinza kilomita 50 na nyingine zilizosalia zitatengenezwa kwa kiwango cha lami, na kumpongeza kiongozi mmoja wa kidini aliyejitolea kujenga kituo cha afya na kukikabidhi kwa serikali kwa lengo la kusaidia wananchi wa Uvinza, ambapo rais alichangia shilingi milioni 10 zilizowezesha kununuliwa kwa vitanda na majokofu. 

Na Mwanaharakati.

No comments: