Hatahivyo rais Magufuli amesema kuwa wananchi wote
waliojenga kwenye hifadhi ya njia ya reli, wajiandae kisaikolojia kubomolewa na
kupisha ujenzi wa reli mpya ya standard gauge, kuwa yeye hapendi kupindisha
sheria, na kuagiza kuwa wakati wa kubomoa, waanzie na nyumba za viongozi wa CCM
wanaopita na kuwadanganya watanzania kuwa wasiondoke kwenye maeneo hayo.
Amesema kuwa ameamua kutumia barabara kutoka mkoani Kagera
hadi atakapofika Dar es salaam, kwa lengo la kuangalia vipande vya barabara
ambavyo vimesalia bila kujengwa kwa lami, na kumwagiza waziri wa ujenzi
uchukuzi na mawasiliano, kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 28 kwa
kiwango cha lami kutoka Kaliua kwenda Urambo.
................BONYEZA CHINI KUSIKILIZA...............
................BONYEZA CHINI KUSIKILIZA...............
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment