Upande wa upinzani katika Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo, umetangaza mpango wa migomo na kuvunja sheria, kujaribu
kumlazimisha Rais Joseph Kabila aondoke madarakani.
Mgomo wa jumla wa siku mbili utaanza
tarehe 8 Agosti, na maandamano ya pamoja yamepangwa
kufanywa baadaye mwezi ujao, katika kila jimbo la nchi.
Katika taarifa yake, upinzani
umesema, ikiwa Rais Kabila hato-taja siku ya uchaguzi ufikapo mwisho wa mwezi
wa Septemba, basi watu waache kulipa kodi kwa serikali.
Muhula wa rais ulimalizika mwaka
jana, na makubaliano yaliyofikiwa baada ya
Kanisa Katoliki kupatanisha, ni kwamba atabaki madarakani hadi Disemba mwaka
huu, lakini rais baadae alisema, hakutoa ahadi yoyote.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment