MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 12 July 2017

PICHA & VIDEO:KAULI KALI YA WAZIRI MHAGAMA KATIKA MAKABIDHIANO YA KITUO CHA AFYA

 MISENYI


Wilaya ya Misenyi iliyopo mkoani Kagera imekabidhiwa rasmi kituo cha afya Kabyaile kilichojengwa kisasa na jeshi la wananchi Tanzania JWTZ baada ya zahanati iliyokuwa maeneo hayo  kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera September 10 mwaka jana.

Baada ya makabidhiano ya kituo hicho kilichokuwa kinajengwa na jeshi la wananchi Tanzania,Waziri wa nchi,ofisi ya waziri mkuu ,sera,Bunge,ajira na watu wenye ulemavu JENISTA MHAGAMA amesema kuwa jeshi limefanya kazi nzuri lakini ukarabati wa vitu vidogovidogo vilivyobakia utafanywa na halmashauri kwa kushirikiana na mkoa huku akisema kuwa fedha ya ukarabati wameshaitoa.

Waziri Mhagama amesema kuwa kwa mkurugenzi na watendaji wa halmashauri ya wilaya Misenyi atakayetumia vibaya fedha hizo hawatamuonea huruma badala yake watakula nae sahani moja kwani fedha hiyo imetolewa kwa ajili ya kukamilisha miundombinu iliyobaki ili kituo hicho kiendelee kuwa katika kiwango bora.
…………………………………..TAZAMA VIDEO YA WAZIRI MHAGAMA…………………………………

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata hiyo wameipongeza serikali kwa hatua hiyo nzuri waliyofikia kwani wamewarahisishia huduma ya afya kwa ukaribu tofauti na ilivyokuwa awali ikiwa ni pamoja na kuhaidi kutoa ushirikiano wa karibu katika kulinda/kutunza kituo hicho.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA UZINDUZI HUO………………






Na Mwanaharakati.

No comments: