MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday 13 July 2017

VIDEO;MAMA ASIMULIA ALIVYOFUKUZWA MUDA MFUPI KABLA YA KUJIFUNGUA

 MISENYI
 
Kufuatia tetemeko lililotokea mkoani Kagera September 10 mwaka jana na kusababisha athari kubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo zahanati ya Kabyaile iliyopo kata Ishozi wilayani Misenyi,baadhi ya wananchi wameeleza changamoto walizokumbana nazo mpaka sasa.

Mkazi mmoja wa eneo hilo Bi,Restuta Isaya amesema kuwa kwa upande wake imemuathiri kwa kiwango kikubwa maana baada ya kutokea tetemeko walitengewa maeneo ya kupata huduma kwa muda wakati jitihada za kurudisha miundombinu zinaendelea.

Aidha amesema kuwa alifika katika eneo hilo wakati anaenda kujifungua lakini walimfukuza na kumwambia aende katika hospital teule ya wilaya Mgana na kuongeza kuwa mtoto alikuwa anakaribia,kitendo kilichopelekea kukodi pikipiki kwa zaidi ya elfu 20 ili awahi huduma Mgana Hospital.

Sanjali na hayo ameipongeza serikali kwa kukamilisha kituo cha afya Kabyaile na kukikabidhi kwa halmashauri,ambapo amewaomba wahudumu watakaofanya kazi katika kituo hicho kuwajali wananchi ili wapate huduma stahiki. 

……….…………………………………….TAZAMA VIDEO HAPA……………………………………………

Na Mwanaharakati.

No comments: