MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 16 July 2017

KAULI YA R.C KAGERA KATIKA KONGAMANO LA FURSA ZA MAENDELEO MKOANI HUMO


July 15 mwaka huu umoja wa vijana wa Bukoba Mpya Economic Inventiveness{BUMEI}ambao ni wazawa wa mkoa Kagera waishio Tanzania na nje ya nchi wamefanya kongamano la fulsa za maendeleo mkoani Kagera kwa lengo kuinua uchumi wa wanakagera kuhakikisha wanasonga mbele kimaendeleo.

Akizindua kongamano hilo mkuu wa mkoa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu amewapongeza kwa wazo zuri walilolileta mkoani humo huku akiwataka kuhakikisha wanafikia malengo yao na si kuishia njiani kwani watu wengi wameleta mawazo ya hivo mkoani humo lakini waliishia katikati.

Meja Jenerali Kijuu amesema kuwa atahakikisha mkoa unawaunga mkono huku akiwasihi kutoingiza siasa katika mpango huo sambamba na kuwashauri wanakagera kuonyesha ushirikiano wa Karibu kwani wanaweza kunufaika kwa mambo makubwa hapo baadae ikiwemo elimu ya Ujasiliamali.

Sanjali na hayo wana Bumei wamewaomba vijana kujitokeza kwa asilimia kubwa kuwaunga mkono maana watwaweza kufaidi kupitia kitu walichokiandaa kwa kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wanaujuzi wa mambo mbalimbali ya kuwainua kiuchumi.
…………………………………..PICHA MBALIMBALI ZA UZINDUZI WA KONGAMANO………………………………


Na Mwanaharakati.

No comments: