MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 17 July 2017

SERIKALI YATAKA KUPELEKEWA MAJINA YA WALIOKWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO BUKOBA {M}



Kupitia kikao cha kujadili taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG manispaa ya Bukoba,imeibuka hoja mbalimbali ikiwemo ya baadhi ya miradi ya maendeleo ndani ya manispaa hiyo kukwama kutekelezwa kwa muda muafaka.

Akisoma hotuba ya mgeni rasmi  kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kagera,mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo amesema kuwa serikali inatakiwa kupata majina ya walioshiriki kwa aina yoyote kusababisha miradi ya maendeleo kushindwa kutekelezwa ili wajue jinsi gani ya kushughulika nao.

Aidha amewapongeza manispaa kwa kupata hati safi kutoka kwa  mkaguzi mkuu wa Serikali kufuatia jinsi walivyotumia fedha kwa awamu hii huku akiwasihi kuendelea kukusanya mapato ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi ya maendeleo iliyokwama.

Kwa upande wake meya wa manispaa ya Bukoba Chief Kalumna amesema kuwa chanzo cha miradi mingi kukwama katika halmashauri ni kutokana na maagizo yanayotoka  ngazi za juu kutaka halmashauri zitekelezre  miradi ya dharura nje ya bajeti.

Kufuatia hali hiyo ameiomba Serikali kuu pindi inapokuwa inatoa maagizo izingatie miradi inayokuwa imeandaliwa na kutengewa fedha kwani tofauti na hapo wataendelea kukwama.

…………………………………….….PICHA ZA BARAZA HILO LEO…………………………………………………..




Na Mwanaharakati.

No comments: