MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 18 July 2017

NCHI YATANGAZA HALI YA HATARI, BAADA YA MAPIGANO YA KIKABILA KUPAMBA MOTO SUDAN KUSINI



Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza miezi mitatu ya  hali ya hatari, kwa kuwataka wananchi wake kusalia nani ya nyumba, kutokana na mapigano ya kikabila kuongezeka nchini humo.

Msemaji wa serikali Michael Makuei, ambaye pia ni waziri wa habari nchini humo, amesema kuwa jeshi limepewa nguvu ya kudhibiti wapiganaji pasipokubagua nani ni nani hasa katika jimbo la Gogrial, na kwamba haki za raia inawezekana zikawekwa kando, ingawa rais amesisitiza wapiganaji wanajivunja.

Vyombo vya habari nchini Sudan kusini vilisema kuwa  watu kadhaa wamekwisha uawa katika mapigano kwenye jimbo la kaskazini ya nchi, ingawa shirika la habari la Reuters halikuweza kujitegemea kuthibitisha idadi ya watu waliouawa. 

Makuei amesema hali hiyo ya hatari pia itatumika katika maeneo jirani ya Tonj, Wau, na Aweil Mashariki, ambapo  Wau ina uzoefu wa mapigano kati ya serikali na waasi watiifu kwa aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar, wa kabila la Nuer.

Sudan Kusini ilitumbukia  katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi Desemba 2013, vikihusisha kwa kiasi kikubwa  askari wa serikali na wanamgambo kutoka makabila ya Dinka na Nuer , na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha huku wengine milioni nne kukimbia makaazi yao.

Mapigano katika Gogrial yaliyomlazimu rais Kiir kutangaza hali ya hatari, yanatekelezwa na   wanamgambo kutoka koo za Apuk na Aguok katika kundi la  Dinka kundi linalomtii rais Salva Kiir.
Na reuters

No comments: