MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 18 July 2017

UTEUZI WA KAMANDA MPYA WA POLISI TAIFA, NA RPC KINSHASA



Rais wa jamhuri wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo  Kongo Joseph Kabila, ameteua mkuu mpya wa polisi na kamanda wa polisi katika mji mkuu Kinshasa, ili kudhibiti usalama unaondelea kuvurugika baada ya kiongozi huyo kung’ang’ania madarakani.

Ongezeko la kubomoa magerezani, utekaji nyara, kuongezeka kwa vurugu za wanamgambo na kufurika kwa uasi tangu Kabila kushindwa kujiuzulu mwezi Desemba, kumeongeza hofu ya taifa la Congo kurejea tena katika machafuko au vita.

Wafungwa elfu 4 walitoroka gerezani mwezi mei mwaka huu katika gereza kuu mjini Kinshasa, na mpaka sasa haijulikani wauaji wa watu wawili na kujeruhi maafisa sita wa polisi katika shambulio katika soko kuu kuu jijini humo siku ya Ijumaa.

Rais Kabila amemteua Dieudonne Amuli Bahigwa ambaye ni jenerali mstaafu na aliyeongoza operesheni mashariki mwa Congo kupambana na kundi la FDLR 2009, kuchukua nafasi ya Charles Bisengimana aliyekuwa  mkuu wa polisi wa taifa la Congo.

Sylvano Kasongo Kitenge KUchukua nafasi ya Celestin Kanyama aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Kinshasa. 

Na Mwanaharakati.

No comments: