Leo July 18, 2017,limezinduliwa jukwaa la wadau wa vyama vya
ushirika mkoani Kagera lenye lengo la kujadili ni jinsi gani wanaweza kutatua
changamoto na kuendeleza ushirika.
Kupitia jukwaa hilo zimebainishwa changamoto mbalimbali
zinazosababisha vyama vya ushirika visisonge mbele,ambapo ni pamoja baadhi ya
wanachama kutorejesha mikopo,elimu ndogo kwa wanachama,mitaji midogo katika
baadhi ya vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja na uhaba wa vitendea kazi kwa
wakaguzi wa vyama hivyo.
Akizindua jukwaa hilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kagera,mkuu
wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo amesema kuwa serikali inahimiza uanzishwaji
wa vyama vya ushirika katika jamii,na kuongeza kuwa watumie vyama hivyo
kuendeleza uchumi kwa wananchi kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia
kipato.
Pia ametoa rai kwa vyama vya ushirika vinavyohusika na
ununuzi wa kahawa kuhakikisha wananunua mazao hayo kwa uaminifu na
kutojihusisha na ubadhilifu wa aina yoyote huku akiwataka maafisa ushirika
wilaya kuwachukulia hatua walanguzi wanaonunua mazao kinyume na utaratibu.
Sanjali na hayo amevipongeza vyama vya ushirika
vilivyoanzisha miradi mbalimbali kutokana na kipato chao na kuwasihi wananchi
kuwa wazalendo kwa kuwaunga mkono kwa vitu wanavyozalisha.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment