Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba leo
amefungua gereza la kilimo la Kitengule lilopo wilayani Karagwe mkoani Kagera lililogharimu
zaidi ya million 100 ambalo ni miongoni mwa majengo yaliyoathirika kufuatia
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo September 10 mwaka jana.
Baada ya ufunguzi huo
waziri Mwigulu amesema kuwa ndani ya
siku tatu waanze mpango wa kurudisha wafungwa waliokuwa wamehamishiwa gereza
jirani la Mwisa ili kupunguza msongamano uliopo ndani ya gereza hilo.
Aidha wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa kuna changamoto ya
wanyama wakali kuingia karibu na makazi yao hali inayowapa hofu kutokana na eneo hilo kuwa asili ya pori,ambapo waziri Mwigulu amesema kuwa changamoto hiyo ameichukua na ataifanyia kazi.
PICHA KATIKA UFUNGUZI HUO..........................................................................
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment