Baada ya ziara ya Rais Magufuli mkoani
Kagera,baadhi ya viongozi nchini Tanzania,leo Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania
IGP Simon Sirro amefanya ziara yake mkoani humo ambapo amekutana na askari wa
mkoa Kagera.
Baada ya mazungumzo na askari
hao,IGP Sirro amesema kuwa miongoni mwa vitu alivyoongea nao ni pamoja na hali
inayoendelea Kibiti juu ya mauaji ya wananchi na kusema kuwa sasa hivi hali
inaendelea vizuri maana wameanza kuwaondoa majambazi ikiwa ni pamoja na kuwaua
huku akiutaka mkoa wa Kagera kutoa ushirikiano ili kukomesha vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa watu hao wanaweza hata kuamia mkoani Kagera
na kusababisha madhara makubwa huku akiwataka wanakagera wote kutoa ushirikiano
pale wanapokuwa na mashaka kwa mtu mgeni ili kama atakuwa miongoni mwa
majambazi hao aweze kuchukuliwa hatua.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment