MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 26 September 2014

MAGAZETI YA LEO 26 SEP 2014

 
 
 
 
 
 
 
Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!! KAULI YA RAIS KUHUSU VYOMBO VYA HABARI TANZANIA




Tanzania inatarajiwa kupata sheria ya Uhuru wa kupata Habari ifikapo Mwezi Februari, Mwaka 2015. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jana tarehe 24 Septemba, 2014 jijini New York alipokuwa mmoja wa wazungumzaji katika mkutano unaohusu Uwazi na ushirikiano kati ya serikali na jamii (Open Government Partnership-OGP). 

Rais Kikwete amesema, rasimu ya muswaada wa Uhuru wa kupata Habari uko katika hatua ya mwisho ambapo wadau mbalimbali wanashauriana na kutoa  maoni tayari kupelekwa bungeni. 

"Muswaada huo unatarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza Mwezi Novemba mwaka huu, na kufikia Mwezi Februari mwakani sheria mpya ya kupata Habari itakua tayari" amesema. 

Mwezi Oktoba Mwaka 2013 katika mkutano wa OGP jijini London, Rais Kikwete alitangaza nia na ujasiri ulioko Serikalini kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na sheria ya Uhuru wa Habari. 

Rais amesema, Uhuru wa Habari ni muhimu kwa wananchi kwa sababu "Ni haki yao ya msingi na kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi yanayofaa kuhusu maisha yao" na kuongeza kuwa "Ni muhimu  wananchi kujua serikali yao inafanya nini kwa niaba yao" amesisitiza. 

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Barack Obama wa Marekani amesema OGP ni ubia kati ya Serikali na Wananchi wake. "Hakuna nchi yenye
majibu yote kwa suala hili la Uwazi katika Serikali, tunahitaji kujifunza kutoka kwa kila mmoja" na kuongeza kuwa ni jambo jema kwa serikali kuimarisha ushirikiano na taasisi za kijamii. 

Viongozi wengine waliochangia katika mkutano huo ni pamoja na Indonesia , Afrika ya Kusini na Ufaransa. Rais Kikwete yuko jijini New York kuhudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) ambapo pamoja na mambo mengine anahudhuria mikutano mingine yenye maslahi kwa  Tanzania. 

Wakati huo huo, Rais Kikwete amekutana na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Bwana Gordon Brown ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa UN kuhusu Elimu ambaye amemshukuru na kumsifu Rais Kikwete kwa kusimamia Elimu nchini Tanzania. 

"Tunataka kukusaidia kufikia malengo ya milenia, tunajivunia mafanikio makubwa uliyoyapata katika elimu" amesema Bw. Brown katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wabia wa maendeleo ambao kwa pamoja wanataka kusaidia Serikali katika kuleta maendeleo na kunyanyua zaidi kiwango cha Elimu nchini. 

Wabia hao ni pamoja na  Shirika la Global Education, Shirika la Watoto Duniani (UNICEF), Shirika la Misaada la Marekani (USAID), wawakilishi wa Serikali ya Uingereza na  Benki ya Dunia. 

Wengine ni kutoka Global Business Coalition na Dubai CARES ambao kwa pamoja wanataka kuinua kiwango cha Elimu ya Msingi na Sekondari kwa kusaidia na kuchangia ili kuboresha zaidi na kuinua kiwango cha elimu nchini. 

Tarehe 25 Septemba, 2014,  Rais Kikwete atahutubia Baraza la Umoja wa Mataifa ambapo hotuba hiyo itaonekana moja kwa moja kupitia UN webcast.
......Mwisho......
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York - Marekani
25 Septemba, 2014
 

Na Mwanaharakati.

Wednesday, 24 September 2014

BREAKING NEWS!!!MAANDAMANAO YA AMANI YA CHADEMA MANISPAA YA BUKOBA YAFANIKIWA

 Maandamano hayo yamefanyika katika kipindi ambapo polisi mkoani Kagera hasa katika manispaa ya Bukoba, wamejipanga na kuzunguka maeneo yote ya mji huo lakini wakashindwa kuwazuia waandamanaji hao, na hatuna uhakikka kama kweli wamewaona.
 

 
Gari la polisi likiwa na askari kadhaa waliojidhatiti tayari kuzuia maandamano ya CHADEMA
Maandamano ya CHADEMA kata kwa taka yamefanyika, ambapo CAMERA yetu imefanikiwa kukutana na msafara wa chama hicho katika kata ya Kibeta, ambapo wameandamana kutokea ndani ya kijiji cha Kibeta na kutokea eneo la Mjuju.
Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!!WASIO NA KAZI KUTIMULIWA MJINI

Mstahiki Meya wa Nanispaa ya Singida, Sheikh Salum Mohammed Mahami ,akizungumza kwenya hafla ya uzinduzi wa shirika la TUSIFO. Hafla hiyo imefanykia katika shule ya msingi Kibaoni na Sheikh Mahami, alitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi ambao hawana shughuli za kufanya mjini,warejee/waende vijijini kwa madai kuwa kwa sasa mazingira ya mjini, sio rafiki kwao tena. Kushoto ni mkurugenzi wa shirika la TUSIFO, Costantino Charles.




MSTAHIKI meya wa manispaa ya Singida, Sheikh Salum Mohammed Mahami, amewasihi wakazi wasio kuwa na shughuli maalum za kufanya mjini, warejee/waende vijijini kwa madai kwamba mazingira ya maeneo ya mjini, sio rafiki kwao.

Sheikh Mahami ambaye pia ni sheikh wa mkoa wa Singida, alisema kuwa mazingira ya mjini sio rafiki kwa watu wasio na kazi maalum za kufanya  kwa sababu gharama za kuishi mijini kwa sasa zimekuwa zikipanda kila kukicha na kupelekea maisha kuwa magumu mno kwa watu wasio kuwa na kipato.

Meya huyo ametoa wito huo wakati akizindua shirika lisilo la kiserikali la Tunawakaribisha Singida Foundation (TUSIFO) linalojishughulisha na kutoa misaada kwa wanfunzi wa shule za msingi na sekondari kwa manispaa ya Singida.

Alisema maisha ya mijini kwa sasa yanafaa zaidi kwa watu wanaofanya kazi  za kueleweka na wafanyabiashara, kwa vile wao wanao uwezo mzuri wa kumudu vema gharama hizo.

“Wafanyakazi na wafanyabiashara, hawa wana uhakika wa kupata chakula mara tatu kwa siku kama inavyotakiwa. Lakini ndugu zetu wasio na shughuli maalum za kufanya,wao hata kupata chakula mara moja kwa siku,kwao ni taabu kubwa”, alifafanua.

Akifafanua zaidi, Sheikh Mahami, alisema pia wasio na shughuli maalum za kufanya, wanalo tatizo la kuzaa watoto wengi bila utaratibu…….familia moja inaweza kuwa na watoto zaidi ya 10 wanaozaliwa mfululizo.
Aidha, alisema uzazi huo usio na tija ,hauzingatii kabisa uwezo wa kuwalea watoto vizuri na ule wa kugharamia masomo.

“Kule vijijini bado kuna maeneo ya ardhi ya kutosha ambapo mhusika anaweza kulima mazao ya kula na ya biashara ,akajipatia chakula cha kutosha na wakati huo huo, akaboresha hali yake ya kiuchumi kwa kuuza mazao ya biashara. Kwa hiyo nawasihi watu wasio na shughuli za kufanya hapa mjini,warudi kijiji mahali wanaweza kujiletea maendeleo na kusomesha watoto wao bila shida”, alisema Sheikh Mahami.

Awali Mkurugenzi wa TUSIFO, Costantino Charles alisema yeye pamoja na wananchama 15 waasasi hiyo, wameamua kuchangishana na kununua madaftari, kalamu, sabuni na sare ili kuwasaidia wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao bila kuwa na matatizo.

“Baada ya kubaini baadhi ya wanafunzi kuacha shule kutokana na kukosa mahitaji hayo,tumemua tuchangishane sisi wenyewe na kuwaondolea kero hiyo wanafunzi kama njia moja wapo ya kuwajengea mazingira mazuri ya kujifunzia”, alisema Costantino.

Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo,kuwaomba wadau wa sekta ya elimu kuiunga mkono asasi hiyo,ili iweze kufikia malengo yake.
Na Mwanaharakati.

LIVE KATIKA UWASILISHWAJI RASIMU YA KATIBA INAYPENDEKEZWA

Katika uwasiliswaji huo, mwenyekiti wa kamati ya uandishi mh Andrew John Chenge, anaendelea kusoma sura mbalimbali za rasimu hiyo.

Katika sura hizyo kuna kipengelea kinachohusu mgombea huru ambapo rasimu hiyo inaonesha kiruhusu kuwapo kwa mgombea huru lakini kukiwa na sharti kuwa mgombea huru hatoruhusiwa kujiunga na chama chochote cha siasa na akifanya hivyo anakuwa amepoteza sifa yake.


Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!! TCRA MITANDAO YA KIJAMII ITUMIKE KULINGANA NA MADHUMUNI SAHIHI






Pamoja na umuhimu nwa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.

Watu hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali toka mitandaoni, kuna mbinu nyingi zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa mbalimbali kutoka kwenye takirishi (Computer) hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao (internet) na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.

Wezi wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares) zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta yake kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia na kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko, kutokana na hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani ndani ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.

Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo kwa kimombo kama ‘Phising’ ambapo ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website hutengenezwa kwa madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote kuhusiana na kitu chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa halisi ya website fulani.

Ili tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa kwa njia ya mtandao kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo makini wakati wote tunapozitumia kompyuta zetu.

Kwaza kabiasa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na hackers ijulikanayo kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu kwa watu tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K vyote kwa pamoja ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika kompyuta na kama ikitokea kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza taarifa zako katika kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa kumtafuta mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.

Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall inasaidia kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers) ambao wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa zilizomo ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za baadhi ya taarifa zako.

Ili kujikinga na wizi wa taarifa zetu katika kompoyuta zetu, tunapaswa kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi virusi (Antivirus) mara kwa mara kwani vizuizi hivyo vimetengenezwa kwa ajili ya kuzuia virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze kuiingia ndani ya mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi cha namna yoyote ile, basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya kisiweze kudhuru kompyuta wakati wote.

Bila shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na tabia ya kuji-update vyenyewe.

Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi ya spyware huwa na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake kama ilivyo kwenye key-logging na Phising au huwa na tabia yakuweka matangazo yasiyo na ulazima katika kurasa Fulani iliyopo katika mtandao wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa usalama wa taarifa za mtu kwani hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi kuwa makini na baadhi ya matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi fulani pasipo malipo kwani mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine huwa na virusi vyenye kuweza kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi yako.

Katika hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya kijamii kuepuka kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa usumbufu wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo ni hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au unaposema (remember me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker kujua nenosiri lako kwa kufanya kitendo kijulikanacho kama (Inspect elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).

Katiko hilo, mharifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti (nyota) kisha anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha anafanya uhariri (editing) katika kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa rangi ya bluu kilichoandikwa neno ‘passoword’, hapo anafuta na kuandika neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’ na akishamaliza kufanya hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda mfumo wa maneno badala ya doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo humuwezesha kujua tarakimu za nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii uliocha wazi.

Njia nyingine ya jinsi ya kujikinga na wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni hasa vibebaji (attachments) toka kwa watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua kwani hata hao hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa malengo yao binafsi.

Pia ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua katika mitandao mingi ya kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na mingineyo kwani baadhi ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names) kuomba urafiki kisha hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.

Kwa upande wa mabenki, ni vema kuachana na mifumo ya kizamani ya kuongozea kompyuta iliyounganishwa na Mashine za kutolea fedha maarufu kama (ATM) au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani hiyo ni hatarishi kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni mifumo ilikwishapitwa na wakati na hata Kampuni yenyewe ya Microsoft imewataka watumiaji kuwa makini nayo kwani haina-updates tena hali inayopelekea kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa mitandao kwa kutumia software za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba taarifa.

Katika matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards) tunapaswa kuwa makini kuepuka kushea namba za siri kwa marafiki au wapenzi na tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo kama nenosiri katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao wamekuwa watu wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.

Ili kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.

Pamoja na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga maendeleo.

Akitoa rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti kwa watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter, Instagram, BBM, LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na kuleta athari kwa jamii.

Alisema matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli, kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye uhalisia.

“Kuna utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi yakugombana kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani inayosababisha kuvunjika kwa amani na kusababisha matusi pande zote,” alisema Mungy.

Mungy aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha amani ya Tanzania.

“Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu iwapo siyo wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine atende kosa,” alisema.

Kwa mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba faini ya kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha miezi mitatu gerezani.

Kutokana na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si vibaya kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani ama kwa lengo la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu wengine, bali inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu mbalimbali duniani kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali japokuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na maelngo ya uwepo wake.


Na Mwanaharakati.