Pichani ni eneo linalopakana na hotel ya PRINCE mjini Bukoba ambpo kumefanyika ujenzi huo holela na kubadili mkondo wa mto kanoni ambo utokea kata za kagondo na nyanga ukikatiza katikati ya mji na kumwaga maji yake ziwa victoria.
Kutokana na ujenzi huu habari za uhakika kuhusu wanaotoa ruhusa ya watu hawa kujenga zinashindwa kudhibitishwa kwani wahusika wa halmashauri wanadai kuwa wananchi wanaamua kukaidi taratibu lakini kwa upande wa wajenzi wenyewe wanadai wamepewa hati za umiliki wa ardhi hvyo wana ruksa ya kujenga maeneo hayo.
Mvua zinapoanza kunyesha mkoani kagera manispaa inaathirika kwani baadhi ya makazi ya watu kama MUKIGUSHA maji uingia hadi ndani ya nyumba zao, kwingine biashara usimama kama inavyoonekana katika picha hapa chini.
Ni vibanda vya wafanyabiashara vimezingirwa na maji na shughuli zimesimama katika eneo la PEDESTRIAN BRIDGE kanoni baada ya mvua iliyonyesha leo Tarehe 14/10/2011.
No comments:
Post a Comment