MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 19 October 2011

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM kata kagondo IGNATUS SIMON amekuta kondoo wake wanne wamechinjwa usiku wa kuamkia leo 19/10/2011 nyumbani kwake Kagondo karuguru katika manispaa ya Bukoba.

Akiongea na mwandishi habari hizi leo asubuhi mwenyekiti huyo amesema baada ya kuamka leo saa moja amekuta wamechinjwa pembezoni mwa zizi la kondoo hao wanne ambapo pia kilichomshangaza kutokuona damu zilizomwagika.

Akifafanua katika hilo amesema ametoa taarifa kituo cha polisi mjini Bukoba ambapo katika maelezo yake hakusita kueleza ugomvi alionao kwa jirani yake ambaye hakupenda kumtaja jina lakini akasema kuwa wamekuwa wakirumbana kwasababu za kisiasa na wakti huo pia wanagombea shamba ambapo kesi yao iko mahakamani.

Kondoo hao wamechinjwa usiku wa kuamkia leo siku ambayo walitarajia kumpeleka mwanasheria ili kukagua eneo linalogombewa hivyo alipofika naye ameshuudia hali hiyo.

Ripoti yake polisi ameitoa na kupewa RB NAMBA BU/RB/5619/2011.

No comments: