MAONESHO YA WIKI YA USALAMA BARABARANI YAMEANZA KATIKA
VIWANJA VYA GYMKANA MANISPAA YA BUKOBA 02/10/2011.
Kubwa nilililoshuhudia pale ni kwamba mabanda yamemuonesha
na kuelezea mawili matatu lakini pamoja na hiyo vifaa mbalimbali vya usalama
vimeoneshwa pamoja na vya kuzimia moto, maelezo ya matumizi sahihi ya barabara
ni vitu vinayoelezwa sit u kwa mgeni rasmi bali wale wote wenye kutembelea
maadhimisho hayo wanafundishwa.
=kwanza tuwashukuru usalama barabarani mkoani kagera kama
utakumbuka alhamisi tulifanya kipindi tukazungumzia mambo mengi kuhusu alama za
barabarani kwakweli nimeona wamejitahidi japo ni kazi zao ila wameweka alama
hizo.
=jambo linguine ambalo limejitokeza ni pale kwenye viwanja
vya GYMKANA huwa kuna dampo la takataka, dampo hilo siku nyingi limejaa
takataka lakini leo dakika chache kabla yta kuwasili mgeni rasmi niemona gari
ambayo naweza kusema kuwa ni ya almashauri yenye nambari STK 1113 aina ya ISUZU
INJECTION ikizoa uchafu.
=Jmbo lingine watanzania tunashindwa kuchangamkia fursa
alafu tunalalamika kuwa hatujaambiwa kampuni ya skania imeskia uwepo wa
maadhimisho ikaamua kufika katika maonesho na vifaa mbalimbali, nimezungumza na
meneja wa scania Tanzania ltd badaye kidogo mtamskia.
No comments:
Post a Comment