MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 1 October 2011

Wakaazi wengi wa manispaa ya Bukoba walimfahamu sana kijana huyu ambaye pamoja na kuwa na mapungufu ya akili, bado alijali sana usafi wake mwenyewe pamoja na kuvaa vizuri, lakini ni miezi kama miwili sasa tangu kugongwa na gari na kupoteza maisha katika barabara ya vibanda vya kuuzia kuku sokoni Bukoba.

Inasemekana aligongwa na gari ya kubeba mchnaga lakini dereva aliyegonga alikimbia na gari hilo na kushindwa kufahamika mara moja, jambo hilo bado lipo kwenye uchunguzi.

Lakini tunabaki na maswali kuwa inakuwaje watu wenye mapungufu wanagongwa na kupoteza maisha lakini matokeo au hatima ya wale walihusika na vifo hivyo hazifahamiki?

Ndani ya mwak huu aligongwa mtoto wa mitaani katika barabara ya uganda katika eneo la uswahili na aligongwa na miongoni mwa vijana wa mjini mfanyabiashara na baada ya kukamatwa aliwekewa dhamana jambo linaloruhusiwa kijamii lakini je hatima ni nini?

No comments: