MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 4 November 2011

AFISA MAWASILIANO TACAIDS Bw RICHARD J. NGAIZA na MENEJA MAHUSIANO TACAIDS GRORY MZIRAY.

Waandishi habari wametakiwa kushirikisha jamii wanayoihudumia ili kushiriki mawazo na kujua matatizo yao kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na meneja mahusiano wa TACAIDS Bi GRORY MZIRAY katika semina ya siku mbili kwa waandishi habari kanda ya ziwa kuhusu maandalizi ya vipindi vinavyohusu ugonjwa wa UKIMWI.

Amesema ugonjwa wa UKIMWI unaendelea kuwepo kwasababu ya wapenzi kuzoeana kwa muda mfupi, jambo linalopelekea kuacha kutumia kinga  baada ya kuwa pamoja katika mapenzi.

Naye Afisa mawasiliano TACAIDS Bwana RICHARD JOSEPH NGAIZA, amesema chombo cha habari cha ndani kinaifikia zaidi jamii ya eneo hilo kutokana na maelewano mazuri ya lugha inayotumika katika maeneo husika.

Semina hiyo ambayo inahitimishwa leo jijini Mwanza imeandaliwa na TACAIDS kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi habari wa vyombo vya ndani (Community Radio) katika kanda ya ziwa ili kuwawezesha kuandaa vipindi kwa ufasaha na ujumbe uweze kufika kwa jamii kwa haraka zaidi.

No comments: