Kamanda wa polisi Kinondoni amesema kifo hicho kimetokea nyumbani kwa msanii huyo baada ya kutokea kutoelewana yeye na rafiki yake wa kike ambaye hakumtaja lakini amesema polisi inamshikilia taarifa zaidi zitaendelea kuletwa kwako.
Naye mwigizaji Dino, amesema ni kwamba kweli
mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo
chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake,
alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae
amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya
kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda
kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba.
No comments:
Post a Comment